Thursday, 8 September 2016

KITA'S FIFTH BIRTHDAY



Happy 5th Birthday Lizbeth-Kita.
Umeendelea kuwa baraka kwetu na tunajivunia sana mwanangu, pia umeendelea kuwa sababu ya sisi wazazi wako kuendelea kuimarika, kuzidi kupendana, na kutupa hamasa ya kupambana na maisha...ni magumu lakini tunayamudu kwani tulishaahidi kutokukuangusha kwa namna yoyote.

Leo umetimiza miaka mitano, unanifanya nikumbuke makubwa yaliyokutokea kwenye mwaka wako wa nne....hata ukija kusoma hichi nachoandika miaka ijayo basi tambua kuwa ni kwenye mwaka wako wa nne umeweza kuandika jina lako, jina la mama yako, jina la mdogo wako na bado unajitahidi kuweza kulimudu langu (nilipewa jina gumu sana kwakweli hivyo nakuvumilia)...pia umemudu kudhihirisha ukali wako kwenye hesabu, mama yako ni mkali sana wa hesabu ila moto wako unaunguza zaidi...endelea hivyohivyo mpaka kuufikia ubingwa. Umeweza kusoma "sounds", "words", na sasa unaunganisha "sentence"...najivunia sana wewe kwakweli. Unanishangaza sana kwa uwezo wako kimasomo, unajua vitu mpaka wakati mwingine natazamana na mama yako na kuanza kucheka (kuashiria kuwa unachojua sasa sisi tulikijua tukiwa wakubwa kidogo)....nilipokea habari nzuri kutoka kwa mwalimu wako kuwa mwakani "utarushwa" darasa kwakuwa unaelewa haraka na vikikaa vimekaa kichwani...nazidi kujivunia wewe, nitaendelea kuwa nawe karibu wakati wote wa kusoma kwako, tutafanya homeworks pamoja kwa miaka mingi sana. Kwa mafanikio yako haya mimi nawashukuru na ukikua utambue mchango wa waalimu wako Teacher Clara na Teacher Getrude, wanajitahidi sana kwakweli na nawashukuru sana. Pia aunt Dora ni wa kushukuriwa sana kwa juhudi zake za kukupelekea chakula shuleni kila siku ili ushibe na kupata nguvu ya kusoma, anaonyesha kukupenda sana kwakweli.
Umekuwa dada mzuri kwa MT na zaidi umekuwa mwalimu wake, tazama leo MT ana count to ten pasi kwenda shule, tazama leo MT anaimba sounds pasi kwenda shule na vingine vingi wamfunza, endelea hivyohivo, ukue ukijua kuna mdogo wako anahitaji uwepo wako katika kila kitu, shikamana naye kila siku pasi kuschoka.
Naendelea kumshukuru mamaako Agatha Nicholaus kwa malezi na upendo, kwake mimi na wewe ni watoto japo kwako mimi ni baba, amejitoa sana kwa ajili yetu, natamani ukue ukiiga matendo mazuri ya moyo wake na zaidi maadili.
Tunatazamia makubwa sana kwenye mwaka wako wa tano kadri Mungu atakavyotujaalia, tutakoleza zaidi upendo wetu kwako, tutaongeza zaidi ukaribu wetu kwako, tutaongeza zaidi muda na wewe ili kwa namna yoyote msingi tulioanza kuujenga kwako uzidi kuwa imara. Tunajinyima kukuridhisha….si tu kwa vile unavyohitaji bali kukuridhisha pia kwa vile tunavyohitaji sisi kwako, tunawekaza pia kwa futere yako na mdogo wako, sala zako kila siku kabla hujafunga macho yako kwakweli zinajibiwa vizuri na Mungu wetu tunayemwamini, kwa mapenzi yake Christmass hii utailia chini ya paa la jasho la wazazi wako…sehemu ambayo ndio utasema rasmi kuwa ni nyumbani, sehemu ambayo ni urithi wenu tukiwa hai na hata ikatokea tumetangulia mbele ya haki…husemwa ukiwa kwako hata ukila dagaa kila siku haihusu, ni kweli lakini nataka nikuhakikishie kuwa tutahakikisha kuwa utakula sausage, dagaa ule kwa kupenda na si kuwa imelazimu (Eee Mungu utusaidie).
Nakuombea kila zuri duniani na mbinguni, nafurahi kuona kila hatua ya ukuaji wako kuanzia unatoa kichwa na kulia kwa mara ya kwanza mpaka sasa umetimiza miaka mitano. Endelea kuwa rafiki yangu wa karibu, rafiki pekee ambaye sina hofu ya kuumizwa naye, rafiki ninayeamini kuwa nikilia atalia nami huku akinifuta machozi, nitautakasa moyo wako wa dhahabu, nataka kuyashuhudia maisha yako ya upendo na furaha.
NAKUPENDA KITA, NAKUPENDA LIZBETH…HAPPY BIRTHDAY.